ARSENAL YAJISHAURI KUACHANA NA ALEXIS SANCHES

KLABU ya Arsenal inafikiria kuachana na mshambuliaji wake tegemeo, Alexis Sanchez ambaye anatajwa kuwaniwa na kocha Pep Guardiola wa Manchester City.

Arsenal wamesema kuwa, iwapo watapewa pauni mil 80, wanaweza kumruhusu Alexis kwenda anakokata.

Dau hilo linawaengua moja kwa moja Bayern Munich ambao walianza kumwania tangu kuisha kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Ujerumani, lakini matajiri wa Manchester City wanaweza kutoa fedha hiyo.

No comments