Habari

ARSENE WENGER ASEMA ALEXIS SANCHEZ HAUZWI, BORA AONDOKE BURE MSIMU UJAO

on

Arsene Wenger amethibitsha kuwa hatamuuza Alexis Sanchez kiangazi hiki – na kuongeza kuwa kama mshambuliaji huyo anaitaka Champions Laegue, basi afanye juhudi ya kuhakikisha Arsenal inafuzu msimu ujao.
Wenger amesema hatajali iwapo msimu huu utakuwa wa mwisho kwa Sanchez ndani ya Emirates Stadium kwa kuendelea kukataa ofa mpya inayokisiwa kufika pauni 300,000 kwa wiki.
Juzi Sanchez alinukuliwa akisema ndoto yake ni kucheza Champions League msimu ujao, kauli iliyofichua mpango wake wa kutaka kuondoka Arsenal.
Mkataba wa Sanches unamalizika mwishoni mwa msimu na iwapo Asrenal itazidi kumng’ang’ania, basi ataondoka bure kiangazi cha mwaka 2018.
Wenger amesema: “Tumecheza Champions League kwa miaka 20 mfululizo, miaka 17 kabla hajaja na miaka mitatu tukiwa naye, kwahiyo kama anapenda sana ligi hiyo, basi ashiriki kuirejesha timu huko.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *