ARSENE WENGER: SANCHES HAJANIAMBIA KAMA ANATAKA KUONDOKA EMIRATES

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Alexis Sanchez hajamwambia kocha wake, Arsene Wenger kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo, gazeti la Daily Mail limeripoti.

Kwa mujibu wa gazeti hilo linasema kwamba Wenger ana imani kubwa kuwa Sanchez ataendelea kukipiga kwenye klabu hiyo msimu ujao na hataondoka kama ambavyo imelipotiwa.

Wenger amebainisha kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile atasaini mkataba mpya na timu hiyo wakati wowote kuanzia sasa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa na Arsenal.

Hata hivyo imeripotiwa kwamba Sanchez angependa kijiunga na wapinzani wa Arsenal, Manchester City kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

Alipoulizwa iwapo Sanchez alimwambia kwamba angependelea kuondoka, raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa hapana.

“Wenger aliongeza: "Wachezaji wana mikataba na tunatarajia kuheshimu mikataba yao, hilo ndilo tunalotaka."

"Kuna mambo watu wanasema bila ya kujua kwamba mchezaji huyo ni mali ya Arsenal, hivyo na yeye anajua fika kwamba bado ni mchezaji wetu halali na hivyo kama kuna chochote kitatokea kwa yeye kuondoka au kubaki ni suala la makubaliano na si vinginevyo."

“Hata hivyo kwangu jambo la muhimu ni kutaka kuhakikisha Sanchez anabaki na sisi tuna matumaini atasaini mkataba mpya wakati wowote kuanzia sasa."


“Kwani hadi sasa hajaniambia lolote kama anataka kuondoka hapa Arsenal hivyo siwezi kusema kuwa ataondoka”.

No comments