ASLAY ADHIHAKI LEBO AKISEMA “ZA KAZI GANI?!”

MSANII wa Bongo flava, Aslay amesema hana mpango wa kuwa chini ya Record Label yoyote Bongo kwa sasa kutokana mipango yake ni mikubwa zaidi.

Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya “Baby” ameiambia XXL  ya Clouds Fm kuwa mipango yake ni kufikia kiwango  cha Diamond na Ali kiba.

“Kusainiwa WCB hapana,  kwa sababu mimi nina ndoto za kuwa zaidi ya WCB au kuwa zaidi ya kitu kingine chochote, naamini nikikaza nitafika kama alipofika Ali Kiba,” amesema na kuongeza.


“Inabidi nikaze niwe mimi kama mimi nitafute njia ya kutoboa nifike level hiyo, yaani sio yeye pekee yake mtu yeyote akisema wanisaini siwezi kukubali sasa hivi,” amesisitiza Aslay.

No comments