AUBAMEYANGA AZIINGIZA VITANI LIVERPOOL NA CHELSEA

MIAMBA miwili katika soka nchini Uingereza, klabu za Liverpool na Chelsea zimeingia katika vita nzito ya kumwania mpachika mabao mahiri wa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Pierre Emerick – Aubameyang.

Taarifa za mitandao mikubwa ya michezo zimeandika leo na jana kuwa usajili wa mwanandinga huyo unaweza kuzitesa zaidi timu hizo kama ataamua kwenda kwingineko.

Gazeti la The Sun limeandika kwamba Liverpool na Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye thamani yake ni pauni mil 65.

Hata hivyo, klabu yake imeamua kumwachia mchezaji huyo atamke mwenyewe anataka kwenda wapi kati ya klabu hizo mbili kubwa.

“Dortmund wamemwambia Aubameyang kuamua anataka kwenda wapi kabla ya klabu hiyo haijaingia kambini nchini Uswisi Julai 24,” limeandika gazeti hilo.

“Tunajua kwamba vita ya kumwania mchezaji huyo ni kubwa na tunajua kwamba kila timu inaweza kufika bei tunayoitaka kutokana na ubora wake, sasa tumemwambia achague wapi anataka,” mmoja wa viongozi wa klabu hiyo amekaririwa na gazeti hilo akisema.

Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa Liverpool ikashinda vita hiyo kwa sababu ya uhusiano wa kocha wa sasa wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Dortmund.

No comments