AUDIO: "FATUMA" KAZI YA KWANZA YA SHAABAN DEDE NDANI YA MSONDO NGOMA

 “FATUMA” kilichorekodiwa mwaka 1979, ndio kibao cha kwanza kabisa kutungwa na marehemu Shaaban mara tu baada ya kutua Juwata Jazz Band akitokea Dodoma International.

Leo wakati tukimalizia msiba wa nguli huyo, saluti5 inakuletea kibao hicho ambacho magitaa yamecharazwa kiufundi zaidi na Kassim Mponda (solo), Issa Ramadhani (rydhym) na hagaika Hussein (Bass).

Mabruki Halfan alisimama imara kwenye ngoma ndogo na tumba zilicharazwa nae Mohammed Atuf, wakati kwenye tarumbeta zimetumika pumzi za Joseph Lusungu na Ramadhani Mnenge katika saxophone.

Sauti za mwenyewe, Dede, Hamis Kitambi na Juma Akida ndio zilizonogesha zaidi wimbo huo ambao unamuasa mwanamke kubaki kwa utulivu nyumbani wakati mumewe akiwa safarini.

No comments