AUDIO: JIKUMBUSHE ENZI ZA TANCUT ALMAS KUPITIA WIMBO “NIMEMKARIBISHA NYOKA”WAKATI mwingine mapenzi, hasa ya ndoa yanahitaji uvumilivu tu lakini wenyewe wahusika ambao ni wanandoa hukutana na masaibu mengi, mojawapo ni hili la kula sahani moja na “mwizi wako”, kama ambavyo Tancut Almas walivyolibainisha kupitia wimbo “Nimemkaribisha Nyoka”.

Mwaka 1987, Kasaloo Kyanga aliyekuwa mwimbaji mwenye sauti kali ndani ya bendi hiyo, alikuja na meseji ya wimbo huo, wakaufanyia kazi na kuwepo kwenye albamu yao ya kwanza iliyokuwa na vibao vingi vitamu kama vile “Kashasha”, “Kiwele”, “Kuwajibika” na “Taulage”.

Baadhi ya wanamuziki walioshiriki kurekodi “Nimemkaribisha Nyoka”, ni mwenyewe Kasaloo, Kyanga Songa, Hashim Kasanga na Mohammed Shaweji (kwenye uimbaji), magitaa ni Shaaban Yohanna Wanted (solo), John Kitime (rithym), Mohammed Ikunji (second solo) na Amani Ngenzi (bass).


Tarumbeta zilipulizwa na Rey Mlangwa na Buhelo Bakari, domo la bata walikuwa Mafumu Bilali na Abdul Ngatwa, ambapo kwenye tumba alikuwa Haruna Rwali.

No comments