MWIMBAJI Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi  asubuhi na kuzikwa Ijumaa mchana, ameacha tungo nyingi nyuma yake ambazo zitaendelea kuishi na kuburudisha sambamba na kuelimisha vizazi na vizazi.

Kaweke Zege Mbinguni alioufyatua mwaka mnamo 1989 akiwa na Bima Lee ni kazi nyingine ya “akili” ya nguli huyo, ambayo inafafanua namna binadamu tusivyotakiwa kumwamini kila tu kwani “mbaya hana alama”.

Waimbaji katika wimbo huu ni yeye mwenyewe Dede, Jerry Nashon “Dudumizi”, Othman Momba na Roy Bashakanako, wakati kwenye magitaa kuna Mulenga (solo), Gama (ridhym) na Mwanyiro (bass).

Said Cuts amesimama vyema kwenye Drums, Saxaphome ni Mafumu Bilali na Kasola Rajab ndie aliyezikong’ota tumba ndani ya “Kaweke Zege Mbinguni” ya wana Magnet Tingisha.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac