AUDIO: MAZOEA YANANIKONDESHA WIMBO ULIOIBEBA MZINGA TROUPE MIAKA YA 1979


MNAMO mwaka 1979 bendi ilioyokuwa chini ya Jeshi la Anga, Ngerengere mkoani Morogoro, Mzinga Troupe “Wana Jiko Moro” iliachia wimbo huu wa “Mazoea Yananikondesha.”

Mtunzi wa wimbo huu ni marehemu Issa mrisho aliyeuimba yeye mwenyewe peke yake mwanzo mwisho kwa sauti ya masikitiko akiwanung’unikia walimwengu wanaoonekana kumkosesha raha katika mambo yake ya mapenzi.

“Mazoea Yananikondesha” ukatokea kukubalika sana miaka ile, hata ukafanikiwa kushika nafasi ya kwanza na yapili kwa miezi miwili tofauti, katika chati za “10 Bora” ya Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).

Mbali na “Mazoea Yanikondesha”, Mzinga Troupe ilibahatika kufyatua vibao vingi kama vile “Sitaki Pombe” na “Usinione Mkimya” ambavyo hata hivyo havikuwakamata sana mashabiki kama hiki cha “Mazoea Yananikondesha.”

No comments