AUDIO: “POLE MAMA JAMES” KIBAO CHA MWENGE JAZZ KILICHOMTAMBULISHA RASMI SHOMARY ALLY KIUTUNZI
MCHARAJI mahiri wa gitaa la solo, Shomary Ally alitokea kujipata umaarufu mkubwa, hasa akiwa na Vijana Jazz, kutokana na tungo zake nyingi kuwa kali kiasi cha mara kwa mara kubeba albamu za bendi hiyo.

Lakini kibao chake cha kwanza kilichomtambulisha rasmi kwenye ramani ya watunzi ni “Pole Mama James” alichokifyatua mwaka 1987 alipokuwa na Mwenge Jazz “Paselepa”.

Katika wimbo huu, mwimbaji Mhina Panduka “Toto Tundu” anang’ara zaidi akiwa amevaa uhusika wa “Mama James”, huku akisindikizwa na akina Fred Siame, Msafiri Haroub na Mabrouk Mohammed.

Solo la masikitiko kwenye “Pole Mama James” limecharazwa na Dancan Njilima, Stephen Maufi (second solo), Shomary Ally (rithym) na Mussa Bomboko (bass).


Drums ni Abdallah Morea na Msimbe kwenye tumba, wakati al za upepo zimekolezwa na Bengwe Simbi, Yustaz Ndunguru waliopuliza tarumbeta, huku Bakari Kubo na Luza Elias wakiwa kwenye midomo ya bata.

No comments