AUDIO: SIKILIZA MOJA YA TUNGO BORA KABISA KUTOKA KWA MAREHEMU SHAABAN DEDE …ni “Toni” ya OSS"TONI" ni miongoni mwa nyimbo ambazo marehemu Shaaban Dede ametunga na kupanga muziki kwa ufundi mkubwa, akitumia mchanginyiko wa chord tatu za kawaida na njia ndogo ya sauti inayojulikana kitaalam kama “minor chord” huku wimbo mzima ukiwa "flat".

Wimbo huu umerekodiwa mwaka 1986 katika Studio za Radio Tanzania Dar es Salaam, wakati Dede akiwa na Orchestra Safari Sound “OSS”, huku waimbaji wakiwa ni mwenyewe, Dede, Muhiddin Gurumo, Khamis Juma na Skasy Kasambula.

Kwenye ala ni Kassim Rashid (Solo), Ally Makunguru (Rythym) na Mustapha Ngosha (Bass), wakati Tarumbeta zimepulizwa na Mubenga Ngoi na Ibrahim Mwinchande wakinogeshwa na mafundi wa Saxaphone Abdallah Kimeza, Majengo Suleiman na King Maluu.


Leo wakati tukiomboleza kifo cha mwenyewe mtuzi Shaaban Dede aliyefariki dunia asubuhi kwenye hospitali ya taifa Muhimbili, Saluti5 inakukumbusha wimbo huu ambao Drums zimecharazwa na Mbaraka Rajab na Immanuel Zagalo kwenye Tumba.

No comments