AUDIO: “UPEPO WA KUSI” KUTOKA KWA SIKINDE UTUNZI WA MWISHO WA ADAM BAKARI

WANAUME wote wanatakiwa kutokuwa na tabia ya kuvamia wanawake ovyo ili kuepuka kugeuzwa mabuzi au hata kufumaniwa na kufanyiwa vitendo vya kiudhalilishaji, kama ambavyo Mlimani Park “Sikinde” wametahadharisha kupitia ngoma yao ya “Upepo wa Kusi’.

“Upepo wa Kusi” ni kati ya vibao viwili vya mwisho kabisa kutungwa na marehemu Adam Bakari “Sauti ya Zege” takriban miaka 20 nyuma na kinapatikana kwenye albamu ya “Overtime” inayokusanya pia nyimbo nyingine kama “Mshangao”, “Maua” na “Overtime” yenyewe.

Mpishano mzuri wa magitaa kwenye wimbo huu ni ufundi wa Kasim Rashid (solo), Mjusi Shemboza (second solo), Huluka Uvuruge (rithym) na John Ngosha (bass), wakati drums zimechapwa na Habib Abbas “Jeff” na tumba zikiwa ni mikono ya Ally Omary Jamwaka.

Waimbaji humu ni watatu tu ambao ni Nassir Lubua, Shaaban Dede na Hussein Jumbe, walioshirikiana kikamilifu kumwimbia kwa karaha mwanaume mpenda wake za watu, wakimtabiria kuwa iko siku  moja tu watamgombea kama mpira wa kona.

No comments