BAADA LACAZETTE ARSENAL SASA YAMPIGIA HESABU JUAN CUADRADO


BAADA ya Arsenal kumalizana na straika wa Lyon, Alexandre Lacazette, anayefuata katika listi yao sasa ni staa wa zamani wa Chelsea, Juan Cuadrado.

Winga huyo wa Juventus hakuwa na jipya Stamford Bridge, lakini Arsene Wenger ambaye dau lake la awali la pauni milioni 22 limegonga mwamba, ana matumaini kuwa anaweza kumbadili kuwa tishio Emirates.

Kituo cha redio cha Colombia, RCN kimeripoti kwamba Wenger ameamua kumfungia kibwebwe staa huyo wa miaka 29, ambaye kwa mujibu wa mtandao wa Metro, Juventus inataka pauni milioni 26.3.

Jose Mourinho alimsainisha Cuadrado kutoka Fiorentina mwaka 2015 wakati akiwa Chelsea, lakini winga huyo wa kimataifa wa Colombia alicheza mechi 13 pekee Stamford Bridge kabla kupelekwa kwa mkopo Juventus.

No comments