Habari

BAADA YA BAKAYOKO KUTUA CHELSEA …NEMANJA MATIC ATAKA ARUHUSIWE KUJIUNGA NA MAN UNITED

on

Kiungo mkabaji wa Chelsea, Nemanja Matic anataka kushinikiza uhamisho wa kwenda Manchester United kufuatia kuwasili kwa  Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco.
Nyota huyo wa kimataifa wa Serbia pamoja na wawakilishi wake wamekuwa mazungumzoni na Chelsea ambapo ameweka wazi utashi wake wa kutaka kuondoka huku akiamini majibu sahihi yatatoka wikiendi hii.
Hata hivyo inaaminika bosi wa Chelsea Antonio Conte bado atahitaji kuwa na kiungo mwingine hasa kutokana na ukweli kuwa Bakayoko atakosa sehemu ya mwanzo wa msimu kufuatia upasuaji mdogo wa goti aliofanyiwa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *