BAADA YA KUMKOSA LUKAKU, SASA CHELSEA YAMFUNGIA KAZI PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG WA BORUSSIA DORTMUND


BAADA ya kumkosa Romelu Lukaku aliyetua Manchester United, sasa Chelsea na baade kuweka nguvu kuhakikisha inamnasa straika Alvaro Morata kutoka Real Madrid, mabingwa hao wa England sasa wanasaka saini ya Pierre-Emerick Aubameyang.

Wakala wa Morata, Juanma Lopez na baba yake, Alfonso Morata, walikutana na maofisa wa Real Jumatatu ya wiki iliyopita kujadili mustakabali wa staa huyo wa miaka 24 na inaaminika mabingwa hao wa Ulaya hawana mpango wa kumpiga bei.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte alimtaka Morata aliyemsaji kutoka Real Madrid mwaka 2014 alipokuwa na Juventus ili kuchukua nafasi ya Diego Costa ambaye hana mipango naye katika kikosi chake kwa msimu ujao.

Lakini sasa baada ya kukatishwa tama ya kumpata Morata, Chelsea imetenga pauni milioni 65 ili kumnasa Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund.


Borussia Dortmund ipo tayari kumwachia mshambuliaji huyo wa Gabon aliyeifungia magoli 120 katika mechi 189.

No comments