Baada ya Manchester United kukamilisha usajli wa Nemanja Matic kutoka Chelsea kwa pauni milioni 40, kocha Jose Mourinho amesema sasa amepata mtu sahihi aliyekuwa akimsubiri kwa hamu kubwa.

Matic kiungo mkabaji, amepewa mkataba wa miaka mitatu na kukabidhiwa jezi namba 31 huku akitarajiwa kuunda ukuta mgumu wa Old Trafford lakini pia kutoa fursa kwa Paul Pogba kuhaha uwanja mzima.

Mourinho amesema: "Nemanja ni mchezaji wa Manchester United na mchezaji wa Jose Mourinho. Yeye anawakilisha kila kitu tunachotaka katika soka; Uaminifu, msimamo, kiu ya mafanikio, mchezaji anayejitoa kwaajili ya timu".

Naye Matic atakayelipwa pauni 140,000 kwa wiki, akasema: "Nina furaha kujiunga na Manchester United. Kufanya kazi na Mourinho kwa mara nyingine tena ni nafasi ambayo nisingethubutu kuikataa."


USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac