Habari

BAADA YA NICHOLAS GYAN, JOSEPH OMOG AAGIZA MGHANA MWINGINE KUTUA KAMBINI AFRIKA KUSINI

on

WAKATI mshambuliaji Nicholas
Gyan ambaye Simba inakusudia kumsajili kutoka Ligi Kuu ya soka nchini Ghana
akitajwa kuondoka nchini humo kuelekea nchini Afrika Kusini ambako wekundu hao
wa Msimbazi wamepiga kambi hatari, taarifa zinasema Simba imevutiwa na straika Mwingine
kutoka Ligi Kuu ya Ghana.
Imedokezwa kwamba Gyan ambaye ni mdogo wake mwanasoka wa timu ya taifa ya
Ghana, Asamoah Gyan anaondoka nchini Ghana katika wiki inayoanza leo kuungana
na wachezaji wengine wa Simba wanaofanya mazoezi nchini huko.
Imeelezwa kwamba
mwanasoka huyo anayeongoza kwa kufumania nyavu katika kikosi cha Ebusua Dwarfs
anakwenda Afrika Kusini baada ya kocha mkuu wa Simba Joseph Omog kuagiza apelekwe huko ili kabla ya kumsajili ampime na kuona uwezo
wake.
Lakini katika kuonyesha kwamba
Simba imepania kufanya makubwa pia inakusudia kumwongeza katika kambi ya
mazoezi nchini humo mshambuliaji mwingine anayecheza katika kikosi cha timu
nyingine inayoshiriki Ligi Kuu ya
Ghana, timu ya Bechem United aitwaye Amed Toure.
Mshambuliaji huyo kwa sasa
anaongoza kwa mabao akiwa amemwacha Nicholas Gyan aliyekuwa anaongoza hadi
wiki iliyopita.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa
Asante Kokoto hivi karibuni aliisaidia klabu yake ya Bechem United kuitandika Bolga Al
Stars kwa mabao 4-0 yeye mwenyewe akitandika mabao matatu mguuni mwake.
“Tunamchukua washambuliaji wawili
katika Ligi Kuu ya Ghana na wote ndio wanaoongoza kwa ufungaji wa mabao, kuna mtu tumempa kazi ya kuimfuatilia Toure, amesema ni mmoja wa watu wa kazi anapokuwa karibu na goli,” amesema mmoja wa watoa habari wetu.
Wakati Nicholas Gyan ni kama
ana asilimia 70 ya kutua Simba, kwa upande wa Toure ambaye ni raia wa Ivory Coast
aliyezaliwa Burikina Fasso anategemewa naye kujaribiwa katika kambi ya Afrika
Kusini.

Kama wawili hawa watasajiliwa
Simba wataungana na Mghana mwinginwe James 
Kotei ambaye ameshaonesha uwezo mkubwa katika Ligi Kuu msimu uliopita
huku kipa Daniel Agyei akidaiwa kutemwa rasmi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *