BADO PAUNI MILIONI 9 MORATA ATUE MANCHESTER UNITED


REAL MADRID imelikataa dau la pauni milioni 70 lililowekwa mezani na Manchester United kwa ajili ya kumsainisha straika Alvaro Morata, ikimtaka Jose Mourinho kufungua tena pochi na kuongeza pauni milioni 9.

Kwa mujibu wa mtandao wa Goal, Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ametaka fedha zaidi ili kumwachia Morata – ingawa straika huyo anatarajiwa kuwasili United Alhamisi.

Straika huyo wa miaka 24 aliye mapumzikoni kwa sasa, hana mpango wa kurudi Real Madrid kwa maandalizi ya msimu, moyo wake akiwa ameuandaa kuhamia Old Trafford, akitaka dili hilo likamilike na kujiunga na kikosi cha United katika ziara ya Marekani mwanzoni mwa wiki ijayo, ambako wataanza kwa kucheza na LA Galaxy Julai 15.

No comments