BARAKA DA PRINCE ADAI AKISALITIWA NA MPENZIWE ITAKUWA SIKU YA WAJINGA DUNIANI

MSANII wa kizazi kipya, Baraka Da Prince amesema kutokana na umaarufu alionao kwa mpenzi wake siku akiambiwa amemsaliti hataamini na pengine itakuwa siku ya wajinga duniani.

Baraka amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Najma Dattan maarufu kama "Naj" na mpaka sasa wameendelea kuwa pamoja.

Baraka alisema kuwa anamwamini sana mpenzi wake na anategemea ndiye atakaekuwa mama watoto wake kwa kuwa anampenda sana.

“Nampenda sana na hata yeye anajua, siwezi kusikiliza maneno ya watu na hata siku ikitokea nikiambiwa kanisaliti sitaamini na pengine siku hiyo itaweza kuwa siku ya wajinga duniani,” alisema Baraka.


Hata hivyo msanii huyo alikana mpenzi wake huyo kuwa mjamzito na kudai wakati wowote ataweka wazi kuhusu hatima ya maisha yao na ndoa.

No comments