BARAKA DA PRINCE ASHAURI WASANII WENZAKE KUPIMA AFYA ZAO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Baraka da Prince amewataka wasanii wenzake wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara.

Akiongea na saluti5, Baraka alisema wasanii wanatakiwa kuwa na tabia ya kuangalia afya zao, hali itakayowasaidia kwenye kazi zao za kimuziki.


“Kucheki afya ni jambo muhimu sana ambalo linatusaidia wasanii ili tuweze kugundua mapema kama tunasumbuliwa na magonjwa ama la ili tukiwa kwenye shoo tufanye kwa ukamilifu mkubwa wa kuburudisha na kuelimisha kwa nguvu kubwa,” alisema Baraka.

No comments