BEKI ALEX SANDRO WA JUVENTUS AWINDWA NA CHELSEA

KAMA ni uchokozi sasa umefika katika kiwango cha juu. Na kama ushakunaku, basi Chelsea wanastahili kusutwa, tena hadharani.

Ukijua mipango hawa jamaa hawa wameweza kusema ni kama hawana huruma.

Mabingwa hao0 wa Ligi Kuu ya England wamesema kwamba hata kama wanaweza kuonekana kama ni wachokozi lakini wanamtaka beki mgumu wa Juvuntus ya Italia, Alex Sandro.

Mwandishi mmoja wa gazeti la The Times amefichua siri kwamba Chelsea wamepania kupeleka pesa ya paun mil 61 kwa ajili ya kumnasa beki huyo raia wa Brazil. Hii ni rekodi ya dunia kwa mabeki.

Mwandishi huyo amesema kwamba anachofanya beki wengine waliochukuliwa na timu za England, wakiwemo Kyle Walker na Benjamin Mendy waliosajiliwa kwa pesa ndefu na Manchester City.

“Chelsea wanamatumaini ya kumalizana kabisa na Alex Sandro, wa Juventus ambaye ni beki wa kushoto.

"Juventus wamejaribu kuzuia beki huyo asiondoke, lakini dau la Chelsea halizuiliki,” amesema mwandishi huyo.

Juventus wamedaiwa kutishia kumzuia beki huyo lakini dau hilo la rekodi kwa beki hapa duniani linaweza kuondoka kabisa kizuizi hicho.

Akiwa na miaka 26, beki huyo amedaiwa kwamba hataki kuongeza mkataba katika kikosi hicho chaTurin na kocha wa Chelsea Antonio Conte amemwomba tajiri wake Roman Abramovich kuto mzigo huo wa maana kwa ajili ya kuibomoa Juventus.

Rafiki yake wa karibu Marcos Alonso ameandika kwenye mtandao wake kwamba beki huyo anatarajiwa kujiunga na Chelsea.

“Hii ndiyo Chelsea tumecheza mechi nyingi za mashindano na kuishinda na hili lakumsajili mmoja wa mabeki bora pia tutashinda” ameandika.


Juventus tayari imempoteza mmoja wa mabeki wake ngunguri Leonard Bonucci aliyehamia kwa wapinzani wao wakubwa AC Milan na sasa wanakabiliwa na hatari ya kuondoka kwa beki huyo mgumu zaidi.

No comments