BELLA NA MALAIKA BAND KUSHAMBULIA MORO JULAI 13 …Ijumaa ni Tanga raha


Mkali wa masauti Christian Bella akiwa na kundi lake la Malaika Band Alhamisi hii, Julai 13 atakuwa pande za Morogoro mjini.

Bella atanyunyiza burudani zake tamu ndani ya kiwanja cha maraha cha Nyumbani Park (Samaki Samaki).

Moja ya zawadi maridadi kwa wakazi wa Moro itakuwa ni ngoma mpya kabisa kutoka kwa Bella inayokwenda kwa jina la “Shuga Shuga”.

Siku itakayofuata, Ijumaa Julai 14 uhondo wa Bella na Malaika Band utahamia Tanga ambapo itaangushwa show kubwa katika ukumbi wa Harbours Club.

No comments