BEN POL KUPIGA KOLABO NA TREY SONGZ

MKALI wa muziki wa R&B nchini, Bernad Paul “Ben Pol” anatarajia kufanya kazi na mkali wa muziki huo nchini Marekani, Trey Songz.

Mipango ya kufanya kazi pamoja imetokana na wimbo mpya wa Ben Pol ambao unajulikana kwa jina la “Tatu” aliomshirikisha Darasa ambapo wimbo huo umeonekana kuvuka mipaka na kuongeza idadi kubwa ya mashabiki.

Ben Pol amesema anafurahi kuona wimbo wake huo ukipokelewa vizuri ndani na nje ya nchi huku baadhi ya wasanii wakijitokeza kufanya nae kazi.

“Nina kolabo nyingi zinakuja kutoka kwa wasanii wa Nigeria na Marekani, ngoma yangu mpya ya “Tatu” imenifungulia njia, ninaamini bado nina nafasi ya kuendelea kuwa na mafanikio makubwa,” alisema Ben Pol.


Alisema miongoni mwa wasanii wa kimataifa anaotarajia kufanya kazi ni pamoja na Chidimna wa Nigeria na Trye Songz kutoka Marekani.

No comments