BENIFICA SASA YATHIBITISHA KUMWEKA SOKONI MARCELO HERMES

KLABU ya Benifica ya Ureno imeweka bayana tetesi za kumuuza mlinzi wa upande wa kushoto, Marcelo Hermes na kusema anaweza akauzwa kwa timu itakayofika bei ambapo wameweka mezani dau la puini mil 33.

Hatua ya klabu hiyo kuweka sawa tetesi hiyo inafuatia taarifa za kwamba timu kubwa za barani Ulaya zimeingia vitani kwa ajili ya kusaka saini ya mlinzi huyo mahiri.

Timu ya West Ham United na Tottenham Spurs ni kati ya vigogo wanaotaka kumsajili wakati wa kipindi cha usajili cha dirisha la kiangazi.

Pamoja na vigogo hao pia timu mbalimbali za nchini Italia nazo zimo katika mbio za kumwania Mbrazil huyo.

Mlinzi huyo kijana amekuwa katika kiwango bora katika msimu huu kiasi cha kuzigonganisha timu mbalimbali, lakini Sky Sports imezitaja West Ham United na Tottenham Spurs kuwa ndizo zilizoonyesha nguvu kubwa kupata saini yake.

Imebainika kuwa Benifica imesisitisha nia ya kumweka sokoni beki huyo baada ya kuondokewa na mlinzi wao mahiri, Victor Lindelof aliyejiunga na Manchester United msimu huu na Renato Sanches aliyejiunga na Bayern Munich msimu wa mwaka jana.

Katika kuhakikisha haimpotezi imeamua kuweka mezani ofa kubwa ya Euro 40 mil ambapo imebainika klabu hizo mbili za premier wanaweza wasipande dau hilo.

No comments