BENJAMIN MENDY WA MONACO NJIA NYEUPE KUTUA MANCHESTER CITY


BEKI wa kushoto wa Monaco aliye kipaumbele katika listi ya wachezaji wanaotakiwa na Manchester City kiangazi hiki, Benjamin Mendy anaonekana kuwa tayari kujiunga na klabu hiyo.


Mendy anahusishwa pia na klabu za Liverpool na Chelsea, lakini gazeti la L'Equipe limeripoti kuwa beki huyo ameuelekeza moyo wake Etihad, ambako anatarajiwa kuungana na Bernardo Silva aliyekuwa naye Monaco.

Katika hatua inayofagia njia ya Mendy kwenda Manchester City, tayari Monaco imekamilisha usajili wa beki wa kushoto Terence Kongolo kutoka Feyenoord kwa pauni milioni 13.

No comments