Habari

BUFFON AMSHAURI GIANLUIGI DONNARUMMA KUANGALIA MATAKWA YA MOYO WAKE NA KUTOJALI KELELE ZA WATU

on

MLINDA mlango mkongwe wa klabu
ya Juventus Gianluigi Buffon amemshauri mlinzi wake katika timu ya taifa ya
Italia Gianluigi Donnarumma kufuata matakwa ya moyo wake na kuachana na kelele
anazopigiwa kwa sasa.
Buffon wenye umri wa miaka 39, aliibuka na ushauri huo kwa kinda Donnarumma mwenye umri wa miaka 18, aliyewaudhi mashabiki wa klabu
anayoitumikia ya AC Milan baada ya kukataa kusaini mkataba mpya.
“Donnarumma afuate kile ambacho
moyo unataka,” alisema Buffon alipokuwa anahojiwa na Sky Sports.
“Nilizungumza naye tukiwa na
timu ya taifa kwa takriban robo saa na nikamweleza awe huru kuamua atakalo
kwenye soka.”

Hata hivyo Buffon ameweka wazi
kuwa hahitaji kuona kinda huyo akichukua ushahuri huo bila kufikiria kwa kina kwani
huenda akazidisha hasira za mashabiki wa Milan ingawa angependa kumuona akitua
Juventus na kuirithi nafasi yake.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *