CHAKACHAKA ASEMA TUZO YA BET IMEMUONGEZEA HESHIMA HADI NJE YA NCHI YAKE

MWANAMUZIKI mkongwe na mwenye mafanikio nchini Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka amesema kuwa tuzo aliyopata kutoka BET imemwongezea heshima ndani na nje ya Afrika Kusini.

Yvonne alipata tuzo ya staa bora na mwenye ushawishi ulimwenguni kutokana na kazi za kijamii anazofanya na muziki kwa ujumla.

“Nilijisikia kuthaminiwa siku niliyopokea tuzo ile, nadhani sasa naweza kuelewa kuwa watu wanathamini mchango wangu kwa jamii iliyonizunguuka,” alisema staa huyo mkongwe.

“Pongezi ni njia pekee ya kuona kile unachokifanya watu wanakithamini na kukumbuka mchango wako,” aliongeza.


Yvonne Chakachaka ni muiongoni mwa wanamuziki wachache waliobaki nchini Afrika Kusini ambao walianza kupata umaarufu tangu enzi za sera za ubaguzi wa rangi.

No comments