CHAZ BABA APATA AJALI MBAYA YA GARI …mchuma wake nyang’a nyang’a


Mwimbaji star wa dansi Chaz Baba, amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya gari leo alfajiri.

Chaz Baba amepata ajali hiyo kilomita chache kutoka Singida mjini akiwa njiani kuelekea Nzega ambapo gari lake aina ya Toyota Porte limeharibika vibaya.

Mwimbaji huyo ameieleza Saluti5 kuwa hakujua nini kilichotokea kwasababu alikuwa amesinzia huku gari likiwa linaendeshwa na rafiki yake.

“Nilishtuka baada ya gari kuacha njia na kwenda kuparamia mawe makubwa. Mwenzangu aliyekuwa akiendesha gari aliniambia kuwa alifanyiwa mchezo mchafu wa kupewa ‘bodi’ na gari kubwa na kupelekea kuingia maporini,” anaeleza Chaz Baba.

Chaz anasema yuko salama ingawa ameumia maeneo kadhaa.
 Hivi ndivyo gari la Chaz Baba lilivyoharibika vibaya
Gari la Chaz Baba linavyoonekana baada ya ajali
 Toyota Porte ikiwa haitamaniki
 Gari limeumia kila upande
Gari la Chaz likibebwa na gari kubwa la mizigo 

No comments