CHELSEA KUJIFARIJI NA AUBAMEYANG BAADA YA KUMKOSA ROMELU LUKAKU

BAADA ya kumkosa Romelu Lukaku aliyejiunga na Manchester United, pengo la Diego Costa katika kikosi cha Chelsea litazibwa na Pierre Emerick-Aubameyang, mtandao wa Sun umeripoti.

Lukaku alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kumrithi Costa anayejiandaa kuondoka lakini wakati Chelsea wakiangaikia usajili wa Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 24, Manchester United waliingilia kati na kumaliza kazi baada ya kuipa Everton pauni mil 75.

Mabosi wa Chelsea wamekuna kichwa na kukubaliana kuipa Borussia Dortmund pauni mil 65 ambazo ni zaidi ya sh bil 182 za Kitanzania ili wamwachie Mwafrika huyo.

Taarifa kutoka Ujerumani zimenyetisha kuwa Dortmund wamekubaliana na dau hilo na watampiga bei nyota wao huyo aliyewafungia jumla ya mabao 120.

Mwanasoka huyo mzaliwa wa Ufaransa amekuwa akizivutia klabu kadhaa za Ulaya katika kila kipindi cha usajili ambapo mbali na AC Milan na PSG, amekuwa pia akifukuziwa na klabu za Ligi Kuu China.

Kocha Antonio Conte ni kama amechanganyikiwa baada ya kumkosa Lukaku kwani tayari alishamwambia Costa hamuhitaji kwenye mipango yake ya msimu ujao.

Mbali na Aubameyang, ili kuziba pengo la Costa anayetajwa kuwa mbioni kurejea Atletico Madrid, pia Conte amekuwa akijaribu kumfuatilia Alvaro Morata ambaye tayari Chelsea wameelezwa kuwa tayari kutumia pauni mil 62 kumsajili.

Conte ameshawanasa Antonio Rudiger beki wa Roma aliyegharimu pauni mil 34 na mlinda mlango Willy Caballero aliyetokea Manchester United.


Pia Conte ameendelea kukazania dili la kuchukua kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko ambaye anatakiwa na Manchester United.

No comments