CHELSEA YAASWA KUANGUKIA WACHINA

KLABU ya Chelsea imetakiwa kuiomba radhi China ili iweze kurejesha uhusiano wake na taifa hilo lenye nguvu kubwa ya kiuchumi.

Baadhi ya wadau wamesema kwamba Chelsea inatakiwa kutambua kuwa China ni sehemu nzuri ya kufanya nao biashara na hivyo kutengana nao ni makosa makubwa.

Mamlaka za masuala ya mawasiliano nchini China inasemekana zimeamuru mitandao ya nchini humo kufuta habari zote zinazohusiana na Chelsea.

Hii inakuja baada ya kiungo Mbrazil wa Chelsea, Kennedy kuposti video ambazo ziliwadhihaki Wachina na kutafsiriwa kama ubaguzi au matusi kwa raia wa nchi hiyo.

Pamoja na klabu ya Chelsea kuomba msamaha kutokana na tukio hilo lakini inasemekana nchini China bado Chelsea wanajadiliwa na wizara husika na adhabu kubwa huenda ikawakumba.

Nchini China wanachukulia siriaz sana masuala ya makosa ya kimtandao na mara zote wamekuwa wakitoa adhabu kali kwa watu wanaofanya makosa ya kimtandao.


Kennedy amewaomba msamaha Wachina lakini pia klabu ya Chelsea iliandika ujumbe kuomba msahama kwa taifa hilo lakini hadi sasa Wachina wamekaa kimya hawajajibu.

No comments