CONTE AFICHUA MAHABA YAKE KWA HARRY KANE

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte ni kama amemfagilia nyota wa Tottenham, Harry Kane baada ya kusema kwamba kama angepata nafasi ya kusajili straika bora duniani, angekimbilia kwake.

Kane, 23, alianza kuonyesha makali yake misimu mitatu ya Ligi Kuu iliyopita na kufanikiwa kutwa kiatu cha dhahabu mara mbili.

Kutokana na ubora huo, Conte amesema kuwa anavutiwa na nyota huyo wa timu ya taifa ya England na akasema kuwa angekuwa chaguo lake la kwanza endapo angeambiwa kuchagua straika.

“Tottenham tayari wana kikosi kizuri endapo wataamua kubaki na wachezaji wote. Kwangu mimi Kane kwa sasa ndio straika bora duniani,” alisema Muitaliano huyo.


“Endapo nitahitaji kusajili straika mmoja nitamkimbilia Kane kwani ni straika aliyekamilika, ana nguvu kimwili akiwa na mpira au hana, yuko vizuri na pia ni mzuri kwa mipira ya juu.”

No comments