CONTE ASEMA FABREGAS ATAKUWA TEGEMEO MSIMU UJAO

KOCHA  Mkuu wa Chelsea, Antonio Conte ameelekeza matumani yake kwa nyota wake, Cesc Fabregas, baada ya kusema kuwa ana imani atakuwa tegemeo kwa klabu katika kipindi cha msimu ujao.

Msimu uliopita licha ya kuwa na mchango mkubwa katika safu ya kiungo nyota alikuwa akishindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mra kwenye kikosi cha kwanza ambacho kiliipa  Chelsea ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu England.

Vile vile  wakati  Eden Hazard akiwa bado anauguza majeraha yake ya enka mwaka huu kunaweza kukashuhuduwa mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji.

"Ni mchezaji mzuri sana ambaye anaweza kucheza vizuri katika nafasi hii  ya kiungo, lakini vilevile ana uwezo wa kucheza namba 10," alisema Conte.

"Ni mfano mkubwa kwa wenzake kutokana na anavyojituma na tabia yake ya kila siku wakati wa mazoezi. Ni lazima ataendelea kuwa hivyo kutokana na kwamba anatufanyia kazi nzuri,”aliongeza kocha huyo.


Alisema kwamba anavyoamini Cesc  kwa sasa ameimarika zaidi tofauti na alivyomkuta wakati alipowasili  Chelsea na akasema kuwa ukimuangalia tangu mwanzo na sasa unaweza kuona jinsi alivyoimarika zaidi.

No comments