CONTE AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUJITUMA KUPIGANIA KUBAKI KILELENI

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte ni kama kawapa somo nyota wake baada ya kusema kuwa ni lazima wajitume zaidi ili kuhakikisha wanabaki kileleni.

Conte alituma salamu hizo baada ya kusaini mkataba mwingine baada ya msimu uliopita kuiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England ukiwa ni wa kwanza tangu Muitaliano huyo ajiunge na klabu ya Stanford Bridge.

Taarifa hizo zimekuja wakati Chelsea wakiwa safarini nchini China na Singapore kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao ambapo watakutana na timu za Arsenal, Bayern Munich na Inter Milan.

“Nina furaha kubwa kwa kuweza kusaini mkataba mpya na Chelsea. Furaha hii inatokana na kwamba katika mwaka wa kwanza tuliweza kupata mafanikio ya kutangaza jambo ambalo ninajivunia nalo. Lakini sasa ni lazima tujitume zaidi ili kuendelea kukaa kileleni,” alisema Conte.

“Tangu mwaka mmoja uliopita nilipowasili mahala hapa mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakinipa msada mkubwa na ni jambo la muhimu kuendelea kupata mafanikio kwa pamoja,” aliongeza kocha huyo.


Kwa upande wake, mkurugenmzi mkuu wa michezo wa Chelsea, Marina Granovskaia alisema kwamba mafanikio ya Conte aliyoyapata msimu uliopita yalikuwa ni makubwa kutokana na kwamba aliweza kulielewa soka la Uingereza kwa uharaka na kuwawezesha kutwaa ubingwa huo wa Ligi.

No comments