Habari

CONTE AWEKA KIGINGI MARCOS ALONSO KUUZWA

on

PAMOJA na kuwepo kwa taarifa
zinazomuhusisha mchezaji wa Chelsea, Marcos Alonso kutakiwa na timu mbalimbali,
lakini kocha Antonio Conte amenukuliwa akisema, hawezi kuuzwa katika klabu
yoyote na kwa dau lolote.
Conte amemwambia mchezaji huyo
raia wa Hispania kuwa bado yumo katika malengo yake ya misimu miwili ijayo
hivyo hawezi kuruhusu aondoke katika kikosi cha Stanford Bridge.
“Alonso ni kati ya wachezaji
niliowaweka katika malengo ya muda mrefu, hawezi kuondoka hapa kwani ana kila
sababu ya kuwemo katika kikosi cha misimu mingi ijayo.”
“Huwezi ukawa na kikosi imara
pasipokuwa na wachezaji wazoefu kama yeye Alonso kwa hiyo sipo tayari kukubali
ofa ya aina yoyote kwa sasa.”
“Yuko kwenye mipango yangu ya
kuimarisha kikosi cha msimu huu.”
“ninachoshukuru ni kwamba ni
mmoja wa wachezaji walio na uzoefu mkubwa wa Ligi, ni msaada mkubwa.”

“Ninampa nafasi katika mechi
kadhaa za kuibeba timu na ninaamini ana uwezo wa kuonyesha kiwango chake cha
misimu miwili iliyopita,” alisisitiza Conte.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *