CONTE: NAPASUA KICHWA KUHAKIKISHA NAKWEPA YALIYOMKUTA MOURINHO CHELSEA

KOCHA Antonio Conte amesema kwamba kwa sasa anajikuna kichwa jinsi ya kuhakikisha  anakwepa yaliyomkuta kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho katika mbio za kuwania ubingwa msimu ujao.

 Msimu wa 2015 Blues  waliweza kutwaa taji hilo wakiwa chini ya Mreno huyo, lakini baadae akafukuzwa Desemba msimu uliofuata baada ya kufanya vibaya na huku timu hiyo ikiwa kwemye nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi.

 Hata hivyo Chelsea iliweza kurejesha taji hilo ikiwa chini ya  Conte na huku ikiiacha nyuma Tottenham  ambayo ilishika nafasi ya pili kwa pointi saba.

 Hata hivyo Conte ambaye amesharejea jijini London, baada ya kumaliza ziara nchini  China na  Singapore  na huku  akiwa ameambulia vipigo kutoka kwa  Bayern Munich  na Inter Milan anasema kwamba kwa sasa anafahamu jinsi presha ilivyo kuhusu kibarua chake.

"Tunafahamu jinsi gani ugumu wa msimu ujao ulivyo na tuna uhakika tunahitaji kuukabili ili yasije yakatokea  kama ya  Mourinho  katika kipindi alichokuwa na Chelsea,"alisema Conte.

"Miaka miwili iliyopita timu ilimaliza ligi kiwa nafasi ya 10 na tunataka hilo lisitokee tena,”aliongeza kocha huyo kabla ya kusema kwamba yeye binafsi anataka pia hilo la miaka miwili iliyopita lisitokee kwa sababu makocha wawili kutoka Chelsea na Leicester  walimuliwa baada ya kutwaa ubingwa na kisha wakaboronga msimu uliofuata.

No comments