COUTINHO AITABIRIA MAKUBWA LIVERPOOL MSIMU WA 2017/18

NYOTA wa klabu ya Liverpool raia wa Brazil, Coutinho ameitabiria makubwa timu yake hiyo kwa kuamini kuwa ina nafasi kubwa ya kupambana kwa ajili ya ubingwa wa premier msimu wa mwaka 2017/18.

Alipoulizwa kwanini ana imani hiyo, Coutinho alijibu kuwa anajivunia ubora wa ocha wao wa sasa, Jurgen Klopp kwani ana mbinu kubwa za kufundisha soka la kisasa.

“Ukiniuliza mimi kwanini ninaamini tu nafasi ya ubingwa, ninaweza kukwambia jambo moja kuwa Klopp ni kocha bora kwa sababu ameibadili timu tangu pale alipopewa jukumu.”

“Liverpool ya sasa ni tofauti na ile iliyokuwa chini ya Brendan Rodgers, kuna tofauti kubwa hata ya namna timu inavyocheza kwa wachezaji kushirikiana dimbani.”

“Tangu atue Anfield ameonyesha mambo mapya ambayo sisi kama wachezaji tunaweza kuwa sehemu ya kuzungumzia mabadiliko haya,” alisisitiza mwanandinga huyo raia wa Brazil.


“Tunacheaz tukiwa na furaha na imani kubwa chini ya Klopp, kama atapewa muda zaidi wa kuendelea kuwa hapa nina imani kuwa kuna jambo linaweza kubadilika na hata timu kurejea katika kiwango cha soka la zamani.

No comments