DANIEL STURRIIDGE ASEMA "NITABAKI HAPAHAPA LIVERPOOL"

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge ameweka wazi mpango wake wa kusalia kwenye klabu hiyo msimu ujao pamoja na kutokuwa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza.

Sturridge amegomea ofa ya kwenda kucheza Ligi Kuu ya China baada ya klabu ya Beijing Guoan kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Jurgen Klopp amemuondoa nyota huyo kwenye mipango yake ya msimu ujao, huku Sturridge akisisitiza kutotaka kuondoka.


No comments