DAVID FERRER AMCHAPA ALEXANDR NA KUTWAA TAJI LA SWEDISH OPEN

BINGWA mara tatu wa michuano ya tenisi ya Davis Cup, David Ferrer, amefanikiwa kutwaa taji la Swedish Open baada ya kumchapa mpinzani wake, Alexandr Dolgopolov, mjini Stockholm.

Ubingwa huo ni mkubwa kwa nyota huyo raia wa nchini Hispania baada ya kushinda kwenye mashindano ya Vienna Open, miaka miwili iliyopita.

Katika fainali hiyo ya jana, Ferrer alimshinda mpinzani wake, Dolgopolov kwa seti 6-4 6-4 na kuwa taji lake la 27 kwenye historia ya maisha yake ya mchezo huo.

Nyota huyo ambaye anashika nafasi ya 46 kwa ubora wa mchezo huo, aliweka wazi furaha yake baada ya kutangazwa bingwa.


“Nina furaha kubwa kwa kuendelea kuweka historia ya mchezo huu, ushindani umekuwa mkubwa sana lakini ninashukuru nimeweza kuandika historia. Niliwahi kufanya hivi miaka miwili iliyopita ninaamini bado nina nafasi ya kuendelea kufanya hivyo,” alisema Ferrer.

No comments