DAVIDO AKANUSHA TAARIFA ZA KUCHEZEA KICHAPO AKIWA NA WASHIKAJI ZAKE

TAARIFA ya msanii Davido na washikaji zake kuchezea kichapo walipokuwa jijini London si za kweli.

Awali ilisemekana kuwa mwanamuziki huyo na wenzake walilazimika kutokea mlango wa dharura katika klabu moja baada ya timbwili la Mr Chris.

Mtandao Plus ulipomfuata meneja wake, Vanessa Amadi ili kujua ukweli wa mambo, mwanadada huyo alisema ni uzushi mtupu.

Huo ni mwendelezo wa Davido kuteka mitandao ya kijamii baada ya tukio la mchumba wake Amanda kujifungua mtoto wa kike Mei 9, mwaka huu.


Pia amekuwa akizungumziwa zaidi kutokana na tabia yake ya kuonyesha maburungutu ya fedha katika mitandao, ukiachana na tukio lake la hivi karibuni la kuunga urafiki na mwanasoka Cristiano Ronaldo kupitia Instagram.

No comments