DE GEA NGOMA NZITO KWA MANCHESTER UNITED NA REAL MADRID

WAKALA Jorge Mendes amekiri kwamba ni kweli ameelekezwa na mteja wake, David de Gea kwamba aharakishe mpango wa kuhama Manchester United na kutua Madrid haraka na akasema kwamba mambo yanakwenda sawa.

“Mambo yanakwenda sawa na kwa kweli kipa huyu sasa anataka kutimiza dhamira yake ya kurejea Hispania,” amesema Mendes.

Wakala huyo amefichua kwamba kama kila jambo litakwenda sawia anadhani msimu huu De Gea atahamia Madrid.
“Ni jambo jepesi tu, nimeshaanza mazungumzo na najua kwamba tutafanikiwa,” amesema.

Baada ya kuidakia klabu ya Manchester United kwa mafanikio makubwa, kipa David de Gea mwenye umri wa miaka 26 hivi karibuni ametamka wazi kwamba amechoka na sasa anataka kuondoka.

Na hafichi hisia zake, De Gea amesema kwamba anafikiri ni wakati wa kutimiza kile kinachosemwa sana kwa maana ya kuhamia klabu ambayo amekuwa akihusishwa nayo kwa muda mrefu.

De Gea amesema kwamba anataka kujiunga na Real Madrid msimu huu na amemwambia wakala wake Jorge Mendes kufanikisha uhamisho wake.

Mwisho

No comments