DEFOE AWAZA KUKIPIGA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA NA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND

LICHA  ya kuwa na miaka mingi katika kibarua chake, straika  Jermain Defoe amesema kwamba amelenga kucheza tena katika fainali za Kombe la Dinia akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya England.

Staa huyo kwa sasa amejiunga na timu ya  Bournemouth akitokea Sunderland, baada yap aka hao weusi kushuka daraja katika Ligi Kuu England,lakini anasema kuwa mawazo yake yote kwa sasa ni kuwamo kwenye kikosi hicho cha kocha  Gareth Southgate kitakachcheza fainali hizo za mwakani zitakazofanyika nchini  Russia.

Wakati wa fainali hizo za mwakani zinafanyika, Defoe ambaye msimu uliopita alifunga mabao  15 atakuwa na umri wa miaka  35  na hiyo itakuwa ni mara yake ya pili kucheza fainali hizo ikiwa ni baada ya kucheza nyingine zilizofanyika nchini Afrika Kusini miaka saba iliyopita.

"Ni jambo la kawaida kwa kila mmoja kutupia jicho kwenye fainali za Kombe la Dunia,"alisema Defoe.

"Kila mchezaji nchini England anapenda kupata nafasi  kwenye kikosi hicho, lakini inategemea na na jinsi unavyocheza kwenye klabu yako,”aliongeza tena.


Alisema kwamba kutokana na hilo ataendelea kuelekeza nguvu zake katika hilo  na endapo atapata nafasi ya kucheza kwenye fainali ndotyo yake itakuwa imekamilika.

No comments