DRAKE AMFUTA WIZKID KWENYE ORODHA YAKE YA MARAFIKI INSTAGRAM

DRAKE amemtibua nini Wizkid? Hilo ndio swali ambalo watu wanajiuliza kwa sasa.

Wizkid kutoka Nigeria anadaiwa kumuondoa kwenye wafuasi wake mitandaoni rapa Drake kwenye mtandao wa Instagram.

Jumapili ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Wiz lakini aliwashtua watu kutokana na ujumbe alioandika katika mtandao huo ambao moja kwa moja ulionekana kumlenga kutokana na kitendo alichomfanyia Drake.

“From today I give no fucks welcome to my world,” ameandika mwimbaji huyo wa Nigeria kwenye mtandao huo.


Ijumaa iliyopita Wizkid aliachia mixtape yake kwenye ngoma ya 12 na wimbo mmoja wa bunus huyo huku Mixtape hiyo ya Sound From the Other Side ikiwa imewakutanisha mastaa kadhaa wa Marekani.

No comments