EVERTON WAZIDI KUMKOMALIA EVERTON

KLABU ya Everton imesema kwamba haina sababu ya kuachana na dili la kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayecheza katika klabu ya Arsenal, Olivier Giroud.

Habari kutoka klabu hiyo zinasema kwamba nyota huyo anayetaka kuondoka Arsenal amekutana na baadhi ya maofisa wa Everton na kufanya mazungumzo ya kina ambayo sasa yanaweza kumwondoa kabisa Emirates.

Ingawaje ana mkataba na timu yake hadi mwaka 2019, lakini mshambuliaji huyo anataka kuondoka kutokana na kukosa namba katika kikosi cha kwanza.

Sio Everton pekee wanaomtaka, pia miamba wa soka nchini Ujerumani, klabu ya Borussia Dortmund nao wameonyesha nia ya kumsajili mpachika mabao huyo.

Marseille ya nyumbani kwao Ufaransa nayo imetajwa kwamba imeingia katika dili la kumnasa mchezaji huyo na habari zinasema kwamba alikuwa arejee Ufaransa lakini mambo kadhaa yamekwambisha.

“Ana uhakika wa kubaki katika Ligi Kuu ya England, bali uhakika zaidi ni kwamba anakwenda Everton ambayo imepania kumsajili,” umeandika mtandao mmoja maarufu wa michezo nchini humo, Inside Futboll.


Mtandao huo umeandika kwamba hakuna shaka kwamba nyota huyo atakuwa katika timu nyingine msimu ujao na mazungumzo yao yanaonyesha kwamba anaondoka Arsenal.

No comments