EVERTON YAHAHA KUFUKIA "SHIMO" LA ROMELU LUKAKU

SASA ni dhamira kuwa, pengo aliloliacha straika Romelu Lukaku ndani ya Everton limeanza kuonekana na klabu hiyo imo katika harakati za kutafuta mbadala sahihi.

Hii ni kwa mujibu wa Ronald Koeman ambaye amekiri wazi kuwa, safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi cha timu hiyo kinahitaji mtu wa kuisaidiana na Wayne Rooney ili kila kitu kiende sawa.

Koeman aliyasema hayo baada ya kushuhudia Everton ikitoka dimbani na ushindi mwembamba dhidi ya timu dhaifu ya nchini Slovakia.

Katika mechi hiyo Everton ili shinda kwa mbinde bao 1-0.
Huu ulikuwa mchezo wa kuanza safari ya mechi za kufuzu kucheza ligi ya Ulaya msimu ujao, ambapo katika mechi hiyo Rooney alionekana kuhaha bira ya kuwa na msaada katika safu ya ushambuliaji.

“Ni dhahiri kuna pengo la Lukaku katika safu ya ushambuliaji. N sahihi kutafuta wa kuziba nafasi hii.”

Rooney yupo fiti lakinio lazima kuwepo na wachezaji wa mfano wa Lukaku,” alisisitiza Koeman.


Lukaku kwasasa anakipiga katika kikosi cha mashetani wekundu wa Old Trafford chjini ya Kocha Jose Mourinho.

No comments