Akiwa katika ardhi ya Tanzania ndani ya dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Wayne Rooney akaifungia Everton bao lake la kwanza tangu arejee timu hiyo akitokea Manchester United.

Katika mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Rooney akaufanya uwanja wa Taifa ulipuke kwa furaha pale alipoifungia Everton bao la kwanza kwa shuti la mita 30 kunako dakika ya ya 37.

Katika mchezo huo ulioisha kwa Everton kuibuka na ushindi wa 2-1, ikawachukua Gor Mahia dakika mbili tu kusawazisha bao kupitia kwa Tuyisenge.

Wakati mchezo ukielekea ukingoni, Everton wakapata bao la ushindi dakika ya 86 kwa mkwaju mkali wa Kieran Dowell.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac