FC BARCELONA KUVAANA NA CHAPECOENSE AGOSTI 7

TIMU ya Barcelona itakutana na Chapecoense katika mechi ya kuwania Kombe la Gamper ambayo itapigwa Agosti 7, mwaka huu katika uwanja wa Camp Nou ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka watu 71 waliopoteza maisha mwaka jana kwenye ajali ya ndege.

Kwa mujibu wa gazeti la Marca, vinara hao wa Ligi ya LaLiga wameamua kuikaribisha Chapecoense kucheza katika mashindano hayo ambayo hufanyika wakati Ligi ikiwa imesimama ikiwa ni mwendelezo wa kuwakumbuka na kuzisaidia familia za wachezaji, maofisa na waandishi wa habari waliopoteza maisha kwa ajaili ya mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Copa Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional.


Katika ajali hiyo, watu watatu tu Neto, Alan Ruschel na Jackson Follmann ndio ambao walinusurika na kuifanya Chapecoense ikiwa katika hali ngumu ya kusuka upya kikosi chake. 

No comments