Habari

FERNANDO SANTOS AJIFARIJI KWA KIPIGO CHA CHILE… atumia ubingwa wa Euro 2016 kukipa “ushujaa” kikosi chake

on

KWA kile ambacho unaweza kusema
ni kama amejiliwaza, kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Fernando Santos amesema
kuwa licha ya timu yake kufungwa na Chile katika mechi ya nusu fainali ya
michuano ya Kombe la mabara, lakini wao bado ni mashujaa kutokana na ushindi wa
fainali za mataifa ya Ulaya “Euro 2016”.
Katika mchezo huo wa katikati
ya wiki uliopigwa mjini Karzan, wachezaji wake watatu Ricardo, Quaresma na Joao
Moutinho mipira yao iliokolewa na mlinda mlango wa Chile, Claudio Bravo na huku
mastaa Alturo Vidal, Charles Aranguiz na Alexis Sanchez wakikwamisha mipira ya
kimiani na kuipa ushindi Chile ikiwa ni baada ya miamba hiyo kushindwa
kufungana.
Hata hivyo, pamoja na mastaa wake
hao kushindwa kufunga, Santos anaonya wasilaumiwe kwa kile anachodai walikuwa
ni miongoni mwa wafungaji walioipa ushindi Ureno wakati ikiifunga Poland katika
mechi ya robo fainali na hivyo kutengeneza mazingira yaliyowafanya waibuke
mabingwa wa fainali hizo za Euro 2016.
“Kwa kushindwa kumtungua mlinda
mlango yalikuwa ni maajabu lakini wachezaji wote watatu walikuwa ndio mashujaa
kwa kuifunga Poland katika mechi ya robo fainali ya Euro 2016,” alisema Santos.
“Na mara zote huwa wakiingia
kifua mbele wachezaji wangu kwani mimi ndie huchukua uamuzi wa kuwachagua,”
aliongeza kocha huyo.

Mwaka jana Cristiano Ronaldo
ndie aliyepiga penati ya kwanza ya mechi hiyo iliyopigwa nchini Marseille,
lakini safari hii hakunyanyua mguu wake, licha ya kushuhudia wenzake wawili
wakikosa za kwanza.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *