FERNANDO TORRES AJIPA IMANI YA KUFANYA MAKUBWA ATLETICO MADRID MSIMU UJAO

STAA Fernando Torres amejipa matumaini kuwa ataifanyia maajabu makubwa klabu yake ya Atletico Madrid baada ya kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja.

Msimu uliopita straika huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania alifanikiwa kuzitikisa nyavu mara nane katika michezo 31 ya Ligi aliyocheza.

Torres alianzia soka lake Atletico kabla ya kuhamia Liverpool lakini ameendelea kuwa kipenzi  cha mashabiki baada ya kurejea akitokea AC Milan ambako alikuwa kipenzi cha mashabiki na ambako alikuwa akikipiga kwa mkopo kwa muda  wa miaka saba.

“Litakuwa ni jambo gumu kwangu kucheza mechi ya nyumbani tukiwa hatupo Calderon,” Torres aliliambia jarida la Dugout.

“Lakini wakati utafika na ipo siku ambayo nitafanya maajabu kuanza kutengeneza kumbukumbu na kucheza soka langu la miaka ya nyuma, nina uhakika kitu hicho kitatokea,” aliongeza staa huyo.

No comments