FUNKE AKINDELE WA NOLLYWOOD MBIONI KUPATA WATOTO MAPACHA

FUNKE Akindele ambae ni mcheza filamu wa Nollywood anatarajiwa kupata watoto mapacha kufuatia ujauzito aliokuwa nao hivi sasa.

Funke ambaye jina lake halisi ni Jennifer anatarajia kupata watoto mapacha baada ya kupewa ujauzito na mume wake, Abdulrasheed Bello ambae ni mtengenezaji wa filamu.

Funke na mume wake walituma posti kwenye mtandao wa Instagram kuonyesha matokeo ya vipimo lakini walifuta baada ya muda mfupi.


“Ameen, nashukuru kwa kunipatia watoto mapacha,” ilisomeka sehemu ya ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa Instagram.

No comments