GARRY MONK ASHIBITISHWA KUWA KOCHA MPYA WA WA MIDDLESBROUGH

KLABU ya Middlesbrough imethibitisha kupata bosi mpya kwenye kikosi chao na tayari wameshaweka bayana kukamilika kwa mazungumzo na kocha Garry Monk.

Garry Monk ambaye ni kocha wa zamani wa Swansea City, kwa sasa ana umri wa miaka 38, anatarajia kutambulishwa rasmi mnamo Jumatatu ya Julai 31.

Kocha huyo aliyewahi kukinoa pia kikosi cha Leeds United tayari amekubali jukumu hilo na atachukua nafasi ya Meneja wa sasa wa Middlesbrough, Aitor Karanka.

“Middlesbrough FC inathibitisha kuwa, Garry Monka ndiye meneja mpya wa kikosi chetu na atatambulishwa rasmi Jumatatu” ilielezwa taalifa kutoka katika tovuti ya klabu hiyo.

Hata hivyo, Boro ameweka bayana kandarasi ya kocha huyo mpya.

Monk alikuwa akitajwa mapema kuchukua nafasi ya Karanka msimu huu baada ya timu hiyo kutofanya kwa mujibu wa matarajio ya klabu kwa msimu uliopita.


Kwa mujibu wa tovuti ya Middlesbrough, meneja huyo mpya atapewa mkataba kulingana na mahitaji ya timu kwa msimu huu, ambapo moja ya malengo ni kutaka imalize ikiwa imo katika nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

No comments